HUDUMA ZA KITABIBU
Posted on: April 26th, 2025Huduma kwa Wagonjwa wa Ndani
- Kupitia taratibu za uchunguzi wa kitabibu utambuzi wa magonjwa hufanyika na kuhakikisha matibabu sahihi hutolewa kwa kila mgonjwa.
- Mzunguko wa kuona wagonjwa Wodini: Hufanywa kila siku ikiwa ni pamoja na Mzunguko mkubwa ambao hufanyika kwa wiki mara moja.
- Mashauriano na Idara nyinginezo kwaajili ya utambuzujumla ki na matibabu ya magonjwa yenye muingiliano wa idara Zaidi ya moja.
Huduma kwa Wagonjwa wa Nje
Idara pia hutoa huduma za kawaida za magonjwa ya ndani na huduma mbalimbali za kibingwa kwa wagonjwa wanaohudhuria kliniki zetu. Kliniki hizi ni kama zifuatazo:
- Kliniki ya kawaida ya magonjwa ya ndani: Huduma ya Matibabu na kufuatilia maendeleo ya matibabu kwa wagonjwa walioruhusiwa na kwa magonjwa tofauti yasiyo ya dharura yenye kuhitaji kulazwa. Mfano: Presha ya kupanda, Baada ya Kiharusi, vidonda vya tumbo, Upungufu wa damu n.k. Hufanya kazi kwa kila siku
- Kliniki ya Sukari: Huduma ya Matibabu na kufuatilia maendeleo ya matibabu kwa wagonjwa wa Kisukari. Hufanya kazi kwa siku zote za kazi katika wiki Jumatatu hadi Ijumaa, ambapo Jumatatu ni mahsusi kwaajijli ya watoto na vijana wenye Kisukari.
- CTC: mahususi kwaajili ya tiba na kujali wateja/wagonjwa na familia zilizoathirika na ugonjwa wa Ukimwi. Hufanya kazi kwa siku zote za kazi katika wiki Jumatatu hadi Jumamosi, ambapo Jumamosi ni mahsusi kwaajijli ya watoto na vijana.
Kliniki ya ngozi: Namna ya matunzo ya Afya ngozi na matibabu ya magonjwa mbalimbali ya ngozi hutolewa.
Kliniki ya Afya ya Akili: Elimu, matibabu na ufuatiliaji wa magonjwa ya Akili hutolewa